TABIA 30 ZA
MWANAMKE ANAYEWEZA KUKUFAA KATIKA MAISHA YAKO.
Mwanamke ni mama mwenye nguvu unajua kwa
nini kwa sababu mwanamke alitoka katika ubavu wa mwanaume baada ya Mungu
kufanya yafuatayo kwa mwanaume
A. Alimpa usingizi mwanaume
B. Alimfanyia upasuaji
C. Damu ilitoka kwa wingi kwa mwanaume
D. Nyama ilitolewa kwa mwanaume
E. Mfupa ulitolewa kwa mwanaume
F. Baada ya kufanyiwa hivyo mwanaume ndipo
mwanamke akaumbwa akatoka mwanaume akakiri na kusema huyo ni mfupa katika mfupa
wangu na nyama katika nyama yangu –hivyo ataitwa mwanamke napenda ujue kuwa
Mwanamke amebeba uponyaji wa mwanaume na mwanaume amebeba vidonda kwa ajili ya
mwanamke
Mwanamke ni mfupa mwanaume ni udongo hivyo
mwanamke ni:
1. Ni nguvu ya mwanaume
2. Ni jasiri
3. Mchapakazi
4. Mwenye kujiamini
5. Tegemeo la familia
6. Mwalimu wa watoto na familia yake
kiujumla
7. Mlinzi wa mwanaume – Bwana akisema
‘’nimefanya jambo jipya duniani mwamke atamlinda mwanaume
8. Chanzo cha baraka ya familia (
nitabariki Uzao wa tumbo lako)
9. Adui wa maadui wa familia (Uzao wa
mwanamke utamponda kichwa nyoka na uzao wa nyoka (shetani ) utamponda kisigino
(mwanzo)
10. Sauti ya familia (Bwana akamwambia
Ibrahimu msikilize mkeo (mwanzo
11. Mponyaji wa familia yake na taifa
12. Mlezi wa huduma (wakamtumikia Yesu kwa
mali zao(Luka8.3-4)
13. Mkombozi wa familia na taifa (kupitia
mariamu mkombozi Yesu kristo alizaliwa (Luka i.29-35
14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa
kufanana naye (mwanzo 2:18)
15. Mwombezi wa familia,huduma na taifa
(Tuwapate wapi wa mama waombolezaji
16. Mficha siri wa Mungu (Rebbeca alificha
ni nani atayekuwa mtawala kati ya watoto wake wawili Esau na Yakobo.Baada ya
kujua umuhimu wa mwanamke tunatakiwa kuangalia kiundani sana tabia 30 za
mwanamke bora sio bora mwanamke tumeumia sana baada ya kuowa watu wasio sahihi
katika eneo lilosahihi mwanamke bora ni mwamuzi wa familia ndio mleta
mabadiliko katika familia mwanamke anayejua kwanini nipo hapa na ninafanya
nini?
Mimi nimefanya utafiki kutokana na vitabu
na maisha yanayotuzunguka nimeweza kugundua tabia 30 za Mwanamke anayeweza
kunifaa mimi na wewe rafiki yangu tuziangalie kwa makini sana na kwa utafiki wa
ndani:-
1. Moyo wa Mwanaume humwamini:
Moyo wa M wanaume humwanini Mwanamke bora
sio bora Mwanamke, Mwanamke bora hujitahidi sana ili aweze kuaminika kwa mume
wake maana Imani ni kitu muhimu sana katika mahusiano, mahusiano yakipoteza
Imani hapo hakuna mahusiano, Mwanamke ana uwezo mkubwa sana wa kujiaminisha kwa
Mwanaume kuwa yeye ni mtu sahihi na chaguo sahihi kwa Mwanaume wake. Moyo ndio
unaothibitisha kuwa huyu ni mtu sahihi au sio sahihi
Moyo ndio unamkubari mtu
Moyo ndio sauti ya mwisho
Moyo ndio chanzo cha upendo
Moyo ndio jibu la maisha yako ya mapendo
Moyo ndio chemichemi ya mapenzi
Moyo ndio unaoamini na kinywa husema yaliyo
maamuzi ya moyo.
Huyu Mwanamke anatakiwa awe na jibu kwa
Mwanaume- Upendo wa kweli hautambuliki kwa muonekano wa mtu bali upendo
huambulika toka moyoni:- Hivyo Mwanamke bora ni Yule anayeweza kuushika moyo wa
Mwanaume na kujiaminisha kwake.
2. Huondoa umaskini
Mwanamke bora katika maisha yako ni Yule
mwenye mawazo mazuri ya kuondoa umaskini katika maisha yako- hana wazo baya,
wengi wao wanatamani kuolewa ili awe na sifa mtaani kuwa ameolewa lakini ni
tegemezi, hana wazo jipya la kubadilisha maisha yako. Hawa sio wanawake sahihi
mawazo yake yanamtegemea mwanaume, wazo lake ni kuzaa watoto hana wazo la
maendeleo, hajui maumivu ya maisha huwa wanarudisha nyuma ndoto zako
kutokutimia kwa wakati wake. Mwanamke bora ni Yule mwenye mawazo ya maendeleo,
mwenye hasira na umaskini mpenda mafanikio huyo ndiyo anafaa kuolewa
3. Kamwe hamtendei Mume wake mabaya
Mwanamke bora yaani niniamaanisha aliye
sahihi ni Yule mwenye moyo safi kwa mume wake,
1. Hawazi mabaya bali mema kwa mume wake,
2. Hawezi kumtendea mume wake mabaya,
3. Hawezi kumuumiza mume wake,
4. Hawezi kumtonesha vidonda mume wake,
5. Hawezi kuumsaliti mume wake,
6. Hawezi kumtendea yasiyo haki mume wake,
7. Hawezi kumchafua mume wake na
kumdharirirsha katika jamiii iliyowazunguka,
8. Hawezikumtukana Mume wake,
9. Hawezi kushabikia maumivu na mateso ya
Mume wake,
10. Hawezi kuwa radhi na maadui wa Mume
wake,
11. Hawezi kuwa jeuri kwa Mume wake,
12. Hawezi kumtendea Mume wake mabaya.
13. Amejaa heshima kwa Mume wake,
14. Adabu,
15. Utu wema anatunza uthamani wa Mume wake
16. Amejaa utiifu na upole kwa Mume wake
17. Amejaa unyenyekevu na uaminifu kwa Mume
wake,
18. Amejaa amani na furaha ya kweli kwa
Mume wake-
19. Anayeshinda uovu kwa wema,
20. Mwenye upendo wa kweli kwa mume wake.
Huyu ndiye Mwanamke unayeweza kumuowa au kuishi naye na ndio sifa ya Mwanamke
anayehitajika katika maisha yako. Mwanamke huyu ataheshimika na kuthaminiwa na
watu na hatakosa upendo wa dhati kutoka kwa Mume wake.
4. Hufanya kazi kwa mikono yake kwa bidii
Mke bora sio bora Mke ni mchapa kazi ni
mtafutaji kwa mikono yake mwenyewe ni mjasiliamali hataki kuwa mzigo wa
familia, kwa mikono yake anajenga, kwa mikono yake anasomesha watoto wake, kwa
mikono yake anatunza familia yake kwa mikono yake anaheshimisha familia, mfanya
kazi kwa bidii asiyechoka usiku na mchana sio mvivu, kwa mikono yake anafanya
hategemei fedha za Mume wake- huyu anafaa kuwa Mke sahihi katika maisha sio
mlinda mlango ni mtafutaji anakufaa sana katika maisha, napenda kukwambia
mapenzi sio kuzaa, mapenzi kama pesa hakuna hutaona udhamani ni wake pesa ni
jawabu la kila kitu sasa Mwanamke anajishughulisha anafaa sana katika maisha
yetu ya leo- mapenzi ni kusaidiana.
Mwanamke sahihi hi Yule anayefanya kazi kwa
mikono yake kwa bidii, Mwanamke ningependa kukushauri kuwa mali za Mwanammme ni
mali za watoto na mali ya Mwanaume ni mali ya watu wengi, leo wanawake wengi
wanateseka sana baada ya waume zao kufa wamenyang’anywa mali zao na ndugu wa
kiume wanateseka sana kwa sababu walikuwa tegemezi kwa waume zao, Mwanamke wa
kweli ni Yule mtafutaji na kuwawekea watoto zake mazingira mazuri ya maisha yao
ya kesho.
5. Yeye ni kama meli ya biashara.
Mwanamke anafananishwa na meli ya biashara
kwa sababu meli ya biashara inachukua bidhaa mbali mbali ndani yake, Mwanamke
amebeba majukumu mengi sana katika maisha yake, mwanamke huyu ni:-
a) Mlinzi wa Mume wake.
b) Mzazi, mlezi mwenye watoto.
c) Mwangalizi mkuu wa familia yake na
mazingira yake
d) Mwalimu Mkuu wa familia yake
e) Adui wa maadui wa familia yake.
f) Muombaji wa familia yake.
g) Kisima cha amani katika familia na ndugu
wanaomzunguka.
h) Chanzo cha Baraka ya familia
i) Mficha siri ya familia- najua unajua
kuwa Mwanamke ndio mficha siri wa familia anajua yote yanayofanyika ndani. Mwanamke
ana majukumu mengi sana huku mtoto analia, baba naye anamwita huku watoto
wanataka kusoma, wakwe wanataka chakula na mavazi huyu anatakiwa kusaidiwa
lakini Mwanamke wa namna hii ndiye anayetakiwa katika maisha yako ndiyo maana
amefananishwa na meli ya biashara malalamiko amepewa yeye matusi yeye, sifa
njema yeye Mwanamke ni gari la familia. Nyumba yenye heshima inamuhitaji
Mwanamke sahihi.
6. Huleta chakula chake toka mbali,
Mwanamke bora hategemei kulishwa na
Mwanaume anasifa yakutafuta chakula chake toka mbali, hulisha familia yake kwa
pesa yake, anahakikisha kuna kila kitu kinachohitajika katika famila yake,
tegemeo la Mume wake Mume humwamini, nguzo ya familia yake, huyu ndiye Mwanamke
anayetakiwa katika maisha yetu, huyu anafaa ni chaguo lililo sahihi katika
maisha yako.
7. Huamka kabla ya mapambazuko.
Mke bora huamka asubuhi na mapema kwa ajili
ya kupanga mambo yake ataamka na kufanya usafi ndani, mazingira yake kiujumla
huandaa chakula mapema hupangilia kazi kwa waliomo ndani mwake hufanya hivi na
wewe fanya hivi sio Mwanamke anayeamka saa tatu (3) asubuhi au saa nne (4)
asubuhi huyo ni mvivu hafai kuitwa Mwanamke bora bali ni bora Mwanamke hafai
hana faida katika kuchangia maendeleo maana hata maandiko matakatifu yanasema
“Siku njema huonekena alfajiri” mafanikio, Baraka, amaendeleo, huanza asubuhi
Mwanamke anyefaa utamwona anaamka asubuhi sana na kupangilia mambo yake sawa,
watu wa nyumbani watakula muda sahihi, wataenda shule wakiwa wamejaa amani
mwenye maneno mazuri juu ya watoto wake na familia yake kwa ujumla. Huyu ndiyo
Mwanamke anayetakiwa katika maisha yako, sio wanaoamka muda wanaopenda,
Mwanaume anaandaliwa chai na mfanyakazi wa ndani, nguo za mume wako
zinanyooshwa na mfanyakazi, maji ya kuoga mume wako yanaandaliwa na mfanyakazi
wa ndani wewe sio Mwanamke sahihi na hufai kuitwa Mke bora wewe ni bora mke.
8. Hufikiri kununua shamba kisha hulinunua.
Mwenamke bora katika maisha hana mtazamo wa
kununuliwa shamba, gari, nyumba na chochote cha maendeleo yake na familia
hufanya mwenyewe akipenda kitu hununua hanunuliwi huyu ndiye Mwanamke wa Biblia
mbunifu wa maisha anayetazama mbali sana kwa fedha yake hufanya maendeleo
makubwa sana katika maisha yake, huyu ndiye Mwanamke bora anayefaa katika
maisha yetu ndiyo Mwanamke anayetafutiwa na watu wenye maendeleo. Anaishi Kwa
Jasho Lake, anategemea jasho Lake Hulima, hufanya kazi ili awezekutimiza ndoto
zake.
9. Huwa tayari kufanya kazi kwa nguvu
Mwanamke bora huwa tayari kufanyakazi kwa
nguvu sana kwa ajili ya familia yake, anajituma kwa bidii kwa kila shughuri
anayoifanya, ni mama mwangaikaji, mwenye kiu ya kutimiliza ndoto yake, mwenye
kutambua wajibu wake kitaifa na kifamilia, mwenye mtazamo wa mbali, mwenye kiu
na maendeleo, mwenye mzigo na familia yake, adui wa umaskini, ujinga na
maradhi, mwenye kujituma kabla ya kutumwa. Huyu ndiyo Mwanamke anayetakiwa kuwa
nayo katika maisha yake, huyu ndiye mama wa kibiblia sio bora Mke ni Mke bora.
10. Mwenye kuthamini shughuri zake.
Mwanamke bora anathamini sana shughuri zake
kuwa zinafaida anaikubali kazi anayoifanya kuwa inafaa, hana tama na kazi za
wengine ana heshimu kazi yake sana, hatishwi na maendeleo ya wengine maana naye
ni Mwanamke anayejiamini sana kuwa hata yeye atafika, mwenye matumaini na Imani
kubwa kwa kile anachofanya. Huyu ndiye Mke anayefaa katika maisha hutasikia
malalamiko, hayupo katika mashindano, hana tamaa mbaya ningependa kukushauri
kuwa mwanamke anayekufaa sio Mwanamke akiona mwenzake amevaa nguo Fulani naye
anataka huyo hakufai ni muharibifu wa maendeleo atakurudisha nyuma kimaendeleo,
tafuta Mwanamke huyo hapo juu.
11. Hufanya kazi hata usiku kwa mwanga wa
taa yake.
Mwanamke huyu mjasiliamali hata usiku
hufanya mambo yake kwa ajili ya maendeleo, hukanda unga wa maandazi, hushona
nguo, vitambaa, hupanga mambo yake kabla ya siku mpya, wenye kutambua wakati
alionao, huyu ndiye Mwanamke anaye kufaa katika maisha yako na ni Mwanamke wa
kibiblia.
12. Asiye mchoyo.
Mwanamke bora sio mchoyo hufungua mikono
yake kwa wahitaji, Mwanamke mchoyo hakufai maana ananyima Baraka katika maisha
yako, Mwanamke mchoyo ni mchawi wa maendeleo, Mwanamke bora ni mtoaji, mwenye
huruma na wahitaji ni mlezi wa wengi, kioo cha fmailia mwenye roho ya msamaha, ni
mama wa wote walio wake na wasio wake, kwa aliyembariki na aliyemlaani, hana
ubaguzi, mwenye moyo wa mama wa kweli, mwangalizi wa wote. Huyu ndiye mwanamke
unaye muhitaji katika familia yako- usifanye makosa huyu ndiyo Mwanamke wa
kibiblia.
13. Hana hofu na maisha ya watoto wake.
Mwanamke bora huwa anahakikisha kuwa
anawaandalia watoto wake maisha mazuri, anawapeleka shule, msimamizi wa
maendeleo yao, mtetezi wa haki zao, anahakikisha watoto wake wanakuwa na nguo,
elimu nzuri, afya nzuri, kazi nzuri na anawaandalia maisha mazuri watoto wake
hivyo anauhakika na maisha yajayo ya watoto wake. Huyu ndiye Mwanamke
anayetakiwa katika maisha yetu.
14. Mwenye kujipenda
Mwanamke bora anajipenda sana,
anajidhamini, ni mzuri sana, mwenye kujikubali mwenyewe, adui wa uchafu, hawezi
huwezi kumkuta mchafu hata watoto wake wanaoga, anapiga mswaki, anapika mafuta
yake mazuri, na anaweka na marashi mwilini ili anukie vizuri sana, anatamanika,
mavazi yake mazuri sana, anamvuto aonekanapo wakati wowote nyumbani na nje ya
nyumba yake, Ua la familia, huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anamvuto wa
kuwanaye karibu, kutembea naye anayethanini usafi wa mwili wake kuanzia
chumbani kwake hadi nje huyu ndiye Mw anamke ninayekushauri uwe naye, huyu
ndiye Mwanamke wa kibiblia.
15. Mume wake hujulikana malangoni.
Mwanamke bora humtambulisha Mume wake
malangoni, Mwanamke ni pazia ya nyumba,
1. Pazia husitiri mambo ya ndani,
2. Pazia hupendezesha nyumba,
3. Pazia mlinzi wa nyumba,
4. Pazia huthaminisha nyumba,
5. Pazia hutambulisha wakaao ndani ya
nyumba,
6. Mwanamke ni pazia ya Mume,
7. Ndiye anayempendezesha Mume,
8. Mlinzi wa Mume
9. Ndiye anaye mthaminisha Mume,
10. Andiye anaye mtambulisha Mume,
11. Kioo cha Mume
12. Mwanamke ni pambola Mwanaume, kama
nyumba ikikosa pazia ni rahisi maadui kutambua vilivyomo ndani na kuvamia,
ikikosa pazia hukaribisha maadui, Mwanamke ni pazia la nyumba ndiyo
anayemtambulisha Mwanaume hata kama huyo Mwanaume ni mjinga Mwanmke anauwezo
mkubwa wa kumuheshimisha Mwanaume mbele za watu, Mwanamke ndio mlinzi wa
Mwanaume. Mwanamke anayejua wajibu wake hawezi kuibiwa Mume hata siku moja
“Sifa ya Mwanaume ni Mwanamke aliye naye”.
16. Mbunifu
Mwanamke bora nimbunifu wa maisha, hayuko
nyuma huweza kufanya kitu na hufanya, mbunifu wa biashara, mitindo ya mavazi,
hubuni na kuwauzisha wafanyabiashara, ni mtundu wa maendeleo, mwenye wazo jipy
huyu ndiye Mwanamke anayehitajika.
17. Mwenye nguvu na kuheshimika
Mwanamke bora ana nguvu za maendeleo mwenye
mali inayopatikana katika mikono yake mwenyewe na mwenye kuheshimika jamii
inameshimu kwa maendeleo yake, inamthamini, inamuogopa, ni kioo cha wa mama
wengine katika jamii inayomzinguka, mke bora anaheshimika na watu, ukiona
unadaraulika unatakiwa kubadilika maana Mke mwema ana nguvu katika jamii na anaheshimika
huyu huyu ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha ya leo.
18. Hucheka afikiriapo wakati ujao (Future)
Mwanamke bora hana hofu na wakati ujao
maana amekweisha udhibiti wakati ujao, Mwamnamke bora hutawala kesho hata kama
hajaingia, hutawala jioni wakati ni asubuhi hivyo hana hofu na mambo ya kesho,
Mwanamke bora anaucheka umaskini, magonjwa na ujinga huandaa mambo yake kwa
wakati aliopo na kwa wakati ujao, huyu ndio Mwanamke anayetakiwa asiyekuwa na
wasiwasi na kesho.
19. Hufungua kinywa Kunena kwa hekima.
Mwanamke bora amejaa hekima kinyuani SOPHIA
- hekima ni kiongozi mzuri sana katika maisha, ni mlinzi, hekima ni mtawala,
hekima ni utajiri, hekima ni heshima,
1. Mwanamke mwenye hekima hashindwi
kuuitawala nyumba yake.
2. Mwanamke mwenye hekima hatishwi na watu
na maneno yao.
3. Mwanamke mwenye hekima ni malkia wa
nyumba yake,
4. Mwanamke mwenye hekima ni mkombozi wa
familia yake.
5. Mwanamke mwenye hekima ni muamuzi wa
haki katika familia yake,
6. Mwanamke mwenye hekima ni mdhibiti wa
maovu katika famila yake.
7. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa
famila,
8. Mwanamke mwenye hekima huondoa hasira
kwa Mume wake.
9. Mwanamke mwenye hekima ni wa kujivunia,
10. Mwanamke mwenye hekima ni mponyaji wa
ndoa yake/ huyu ndiyeMwanamke anaye tafutwa katika maisha yetu rafiki wa wote
huyu ndiye Mwanamke anayehitajika katika maisha.
20. Huwashauri wengi kwa wema.
Mwanamke bora ni mshauri mzuri kwa wengine,
mwenye kushauri mema wala sio mabaya kwa watu waliomzunguka yaani ni mponyaji
wa familia za watu wengi hata taifa, ushauri wake hauna madhara kwa watu,
kimbilio la wengi, sio mwenye mwenye kuharibu ndoa za watu, mchonganishi,
mshirikina, muongo hapana, Mwanamke anatakiwa kutoa ushauri mzuri kwa wengi
huyu ndiye Mwanamke tunayemuhitaji wengi.
21. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani
mwake.
Mwanamke bora anakuwa makini sana na kila
kitu kinachoendelea au kutendeka katika nyumba yake anakuwa mwangalifu sana mna
mambo ya nyumbani kwake kwa sababu yeye ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yke,
anatakiwa awe na muda wa kutosha na nyumba yake, hapendi ujinga nyumbani mwake,
mahali pa kuonya anaonya, mahali pa kufundisha nafundisha, yeye ndiye mratibu
mkuu wa yote yanayotendeka nyumbani, yeye ndiye kiongozi wa nyumba yake,
mtendaji mkuu wa nyumba yake ndiye mjenzi wa familia bora hivyo Mwanamke kama
huyu anyejua mjukumu yake ndiye anayetakiwa katika maisha yetu, sio kila
Mwanamke umuonaye anafaa.
22. Kamwe hakai bure hata kidogo
Mke bora hakai bure lazima atakuwa na kitu
cha kufanya, huwezi kumkuta kwenye vikao vya umbea, anazunguka zunguka kwenye
nyumba za watu, maana ana mambo ya kufanya hakai bure hata kidogo ni mchapa
kazi, anajituma, mbunifu wa mambo, anautaratibu wa maisha yake. Mwanamke ambaye
yupo yupo tu huyo hatufai,ni chanzo cha matatizo, umbea, muongo, tafuta
Mwanamke anayechapa kazi yuko (busy) na shughuri za kifamilia, kiofisi mwenye
maendeleo huyo ndiye Mwanamke anayefaa katika maisha.
23. Watoto wake huamka na kumshukuru.
Mke bora watoto wake wanafuraha naye,
wanamshukuru sana mama yao, maana amewajengea maisha mazuri amewafundisha mambo
mazuri, amewalea vizuri, watamuheshimu sana mama yao na kumpenda, watamlinda na
kumtunza mama , mama wa kweli husifiwa na watoto wake, watoto wanajisikia amani
wanapokuwa naye, mwenye maadili mema mbele ya watoto wake,. Mfano wa kuigwa kwa
mambo mazuri anayowatendea watoto wake hivyo shukurani hazitaweza kundoka
midomoni mwa watoto wake huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa.
24.Mume huimba sifa zake
Mke bora Mume wake humsifia kwa sifa njema
Mume hutangaza uzuri wa Mke wake, hutangaza mtendo mazuri ya Mke wake,
hujivunia na anajisikia bahati kuwa na mke kama huyo, mwenye tabia njema,
mtiifu, mpole katika maisha yake mwenye kujiheshimu, anyempenda mume wake na
watoto zake, msema kweli, mlinzi mwaminifu, Mwanamke mwenye maendeleo huyu
ndiye Mwanamke anayetakiwa katika maisha yetu aliyekubarika katika moyo wa Mume
wake mpenzi.
24. Mwenye kumcha Mungu
Mke bora ni Yule mcha mungu anayempenda
Mungu mtu wa Ibada mwenye hofu ya Mungu anayeichukia dhambi, mpenda maombi na
Neno la Mungu huyu ndiye Mke sahihi katika maisha, mwenye mzigo wa maombi kwa
ajili ya Mume wake na watoto wake na wote waliomzunguka huyo ndiye chemichemi
ya mabadiliko ya familia, mleta ukombozi wa fmailia huyu ndiye Mwanamke
anayefaa katika maisha yetu ya leo.
25. Mwenye kupenda elimu.
Mke bora ni Yule anyependa Elimu. Elimu
imegawanyika katika sehemu mbili. Kuna Elimu inayopatikani mashuleni na Elimu
inaopatikana katika mazingira unayoishi, wazazi na jamii iliyokuzunguka Mke
bora anapenda kujifunza mazuri kwa wengine, mafanikio yao, sio mjuaji, yupo
tayari kurekebishwa na kubadilika, anayekubari kushauriwa huyo ndiye Mwanamke
anayefaa maana ni msikivu na mpenda mabadiliko yenye faida
26. Huandaa chakula kwa familia yake.
Mke bora ni mpishi mzuri wa chakula katika
familia yake hategemei wafanyakazi yeye ni Mwalimu wa wengine mume humsifia
Mkwa kwa mapishi yake mazuri nay a usafi wa hali ya juu sana . mpendwa najua
unajua kuwa kuna baadhi ya wake za watu hawajui kupika, sio mbunifu wa mapishi
mchafu katika maandalizi yake huwa ni wake wasio bora, wanavunja nyumba zao,
tafuta Mke ambaye hana chakula cha kukariri bali bali ni mbunifu wa mapishi ni
msafi anayejipenda mwalimu wa mapishi huyo ndiye Mwanamke anayetakiwa katika
maisha yetu ya leo.
27. Mwenye sifa njema.
Mke mwema anasifa njema katika jamii
iliyomzunguka hana tabia za uzinzi na uasherati, hana tabia ya ulevi na matusi,
hana tabia ya umbea na uchonganishaji, hana tabia ya kiburi na jeuri Mke mwema
ni rafiki wa watu wengi amejaa shukrani na hana mawazo mabaya Mke bora
hutambulika na matendo yake katikajamii inayomzunguka.
28. Mwenye kudhamini na kutunza upendo.
Mke bora anajua maana ya upendo na gharama
zake, anajua maumivu na vidonda vya mapenzi, anajua nguvu ya upendondani ya
mtu, anatambua hisia kali ya upendo, Mwanamke wa namna hiyo hataweza
kukusaliti, atakuheshimu na kukupenda kweli kutoka moyoni mwake hatagawa upendo
wakko kwa wengine, atalinda penzi lake kwa ajili yako, anaheshimu mwili wake
huyu ndiye Mwanamke anayetafutwa anayejua kwanini umempenda yeye na umewaacha
wengine mwenye tabia njema. Huyu ndiye Mama wa familia bora sio bora familia.
29. Mwenye wivu wa maendeleo
Mke bora ana wivu wa maendeleo hana wivu wa
kijinga unaoweza kusababisha amani katika ndoa kuondoka .Mwanamke ni mponyaji
wa ndoa yake ni kweli Mwanamke anatakiwa awe na wivu kwa Mume wake lakini
vilevile lazima awe na Imani na Mume wake, kuna wivu unaoweza kuharibu amani ya
nyumba lakini kuna wivu unaoweza kujenga nyumba. Inategemea Mama ana wivu wa
namna gani sio wote walio karibu na Mume wako, wako katika mahusiano na Mume
wako, Mwanamke bora hufanya utafiti wa jambo na kuwa na uhakika naolo na
huliwasilisha kwa hekima sana. Wivu ni mzuri ukitumiwa vizuri na pendo la kweli
lina wivu lakini uwe wa maendeleo katika maisha yenu.
Mpendea wangu huo ndio utafiti wangu kuhusu
mwanamke anayefaa katika maisha yako nimetumia kitabu cha (Mithali 31:10-31)
(Goodnews bible)
Kumpata Mwanamke bora sio kitu rahisi
lakini kupitia mafundisho ya vitabu kama hivi, vitafungua ufahamu wako mkubwa na kumtafuta Mke sahihi kimungu-
kibiblia
By NYGONDE CHACHA NYAGONDE
No comments:
Post a Comment