1.0
UFUGAJI WA SAMAKI
Ø Ni
kitendo cha kuzalisha samaki katika mabwawa, matenki au Mifereji kwa lengo la chakula au kujipatia kipato
1.1
UMUHIMU WA UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji wa samaki unazo
faida mbalimbali ambazo ni:-
Ø Kujipatia
chakula bora na cha kutosha kwa ajiri ya familia na jamii.
Ø Njia
bora ya kujiajiri na kujiongezea kipato kutokana na mauzo ya samaki.
Ø Hutoa
fursa ya matumizi ya ardhi isiyofaa kwa ajili ya kilimo.
Ø Ufugaji
wa samaki hutoa nafasi ya kilimo mseto cha samaki na mazao/mifugo kwa wakati
mmoja katika eneo moja, hivyo kutoa mavuno mengi.
1.2.0 MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA
KUANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI;
1.2.1Mtaji
Ø Mkulima
anashauriwa kuhakikisha kuwa ana mtaji kabla hajaamua kufanya ufugaji wa
samaki, kiwango cha mtaji kitategemea ukubwa wa mradi husika.
1.2.2
Soko
Ø Ni
vyema kujua upatikanaji wa soko pamoja na washindani wako kabla ya kuanzisha
shughuli hii, japo kwa nchi yetu soko la samaki ni kubwa sana, hii inatokana na
uhitaji mkubwa wa samaki katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
1.2.3
Elimu
Ø Mkulima
anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu
samaki na jinsi ya kufuga ili aweze kuendesha mradi kwa urahisi, hivyo mkulima
anaweza kutafuta mtaalam kutoka vyuo vya serikali au binafsi.
1.2.4
Upatikanaji
wa mbegu(vifaranga) pamoja na chakula.
Ø Mkulima
anashauriwa kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbegu bora na chakula cha kutosha
kwa ajili ya kulisha samaki.
1.2.5
Eneo
la kufugia samaki
Ø Ni
vyema pia kutafuta eneo zuri kwa ajili ya kuchimba bwawa la kufugia samaki kwa
kuzingatia upatikanaji wa maji
kwa wakati wote wa msimu wa ufugaji, aina ya udongo, usalama na upatikanaji wa
miundombinu husika (barabara, nishati ya umeme).
2.0 AINA
YA SAMAKI;
2.1 Utafiti
umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato
[tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawa kulinganisha na aina
nyingine.
2.2 Samaki
wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri
katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na
chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani,
hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki
hawa ni tamu na yenye ladha nzuri.
2.3 Kuna
aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato
mweupe na Sato wa Mwanza.
Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji
chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya
plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za
samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.
2.4 Sato
wa Mwanza ni moja kati ya aina ya
tilapia inayoshairiwa kufugwa na wataalamu wengi kwa kuzingatia sifa mbalimbali
tofauti na aina nyingine.
3.0 ENEO
LINALOFAA KWA UFUGAJI WA SAMAKI AINA YA SATO:
3.1.1 Upatikanaji wa maji
3.1.1 Maji
ni moja ya hitaji muhimu katika ufugaji wa samaki. Eneo litafaa kwa ufugaji wa
samaki ni lenye maji ya kutosha kuendesha shughuli zote za ufugaji kwa kipindi
husika.
3.1.2 Chanzo cha maji kwenye bwawa
kinaweza kuwa; mto, mfereji wa kumwagilia, au chemi chemi. Bwawa linahitaji
maji mengi na sio rahisi kujazwa na ndoo. Ili kuhakikisha kuwa bwawa linakuwa
na maji ya kutosha muda wote, chanzo cha maji cha faa kuwa cha kuaminika.
3.1.3 Kama
mkulima ana maji ya kujaza kwenye bwawa kwa msimu, inawezekana pia kufuga
samaki. Lakini mkulima ahakikishe anapanda vifaranga vya samaki mwanzo wa msimu
wa maji. Hii itatoa fursa kwa samaki kukua hadi kufikia kiwango cha kuvunwa
kabla ya maji kukauka.
3.1.4 Kama
wakulima wanatumia chanzo kimoja cha maji ni muhimu kuanzisha utaratibu ambao
utawezesha wakulima wote kutumia maji hayo bila matatizo. Wafugaji wa samaki
wanaweza kujaza mabwawa wakati wowote kutegemea ni kipindi gani maji hayatumiki
sana kwa matumizi mengine.
3.1.5 Ili
kuhakikisha kwamba bwawa halitumii maji mengi, ni muhimu kuimarisha kingo za
bwawa kwa kushindilia vizuri udongo wakati wa ujenzi wa msingi wa bwawa. Hii
ina maana kwamba udongo lazima uwe na kiwango kikubwa cha mfinyanzi. Udongo
ambao unatumika kutengenezea vyungu au kufyatulia matofali ni mzuri sana kwa
shughuli hii. Kama udongo hauna ufinyanzi wa kutosha bwawa litapoteza maji kwa
urahisi na italazimu
kuongezwa kwa maji mara kwa mara.
3.2 Aina ya udongo
3.2.1 Inashauriwa
kuwa udongo wa tifutifu au mchanganyiko wa tifutifu na mfinyanzi ambao una
uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu unafaa zaidi kwa ufugaji wa samaki.
3.2.2 Udongo wa kichanga sio mzuri katika
kushikilia maji lakini eneo lenye udongo wa aina hii linaweza kutumika kufuga
samaki ikiwa mbinu mbalimbali zitatumika.
Zingatia
·
Kwa eneo lenye kichanga lakini lina
upatikanaji wa maji ya kutosha mkulima anaweza kutumia mbinu ya kujaza mchanga
kwenye mifuko ya saruji iliyokwisha kutumika na kuipanga kwenye kingo za bwawa
ili kuimalisha kuta za bwawa. Kwakuwa mifuko inaweza kuoza kutokana na maji,
inashauriwa ibadilishwe endapo kingo za bwawa zitaanza kumomonyoka na kuongeza
tope ndani ya bwawa.
·
Karatasi ngumu ya nailoni yaweza pia
kutumika kuzuia kupotea kwa maji na kulinda kingo za bwawa kumomonyoka.
·
Ujenzi wa kuta za bwawa kwa mawe au
bwawa zima ni njia bora zaidi japo ni gharama ukilinganisha na mbinu nyingine.
Mifuko
picha ya bwawa liliotengeneza kwa
karatasi ya nailoni
nylon
kuta
3.3 Mambo mengine ya kuzingatia katika
uchaguzi wa eneo la kufugia samaki
3.3.1
Eneo liwe na mteremko kiasi ili
kusaidia shughuli nzima ya uingizaji na utoaji wa maji kwenye bwawa. Nguvu
nyingi zitatumika kuchimba bwawa eneo lenye mwinuko mkali na ni vigumu kujaza
au kutoa maji kwenye bwawa lililochimbwa eneo la tambarare
3.3.2
Eneo linatakiwa kuwa na miundombinu bora
na lenye kufikika kwa urahisi ili kusaidia usafirishishaji wa mazao, vifaranga
na mahitaji husika.
3.3.3
Eneo lisiwe na historia ya mafuriko, hii
ni hatari kwa kuwa mafuliko yanaweza kuvunja kingo za bwawa hivyo kuhatarisha
shughuli ya ufugaji.
3.3.4
Eneo lisiwe karibu na maeneo hatarishi
kama vile viwanda, shughuli za kilimo zenye kutumia kemikali ili kuzuia madhara
ya kikemikali.
3.3.5
Eneo liwe karibu na mmiliki ili
kuimalisha ulinzi na urahisishaji wa uendeshaji wa shughuli za uzalishaji.
7.0 VYANZO VYA MAJI KWA UFUGAJI WA SAMAKI;
7.1 Ni vyema mkulima kuchagua chanzo cha maji
kinachofaa kulingana na mazingira yake pamoja na manufaa kwa mkulima.
7.2 Unaweza kutumia maji ya kisima, chemichemi,
ziwa, mto na bomba kwa kuzingatia sheria na taratibu husika.
7.3 Matumizi ya maji ya bomba katika ufugaji
samaki ni lazima uzingatie ushauri wa kitaalamu. Lakini mambo yafuatayo
yanaweza kumsaidia mkulima kutumia maji ya bomba kama chanzo cha maji; kabla ya
kuweka samaki maji yawekwe kwenye bwawa kwa takribani siku kumi, hii itasaidia
kuondoa chlorini kwenye maji, mbolea na tembe za vitamin c zaweza pia kutumika
kuharakisha uondoaji wa chrolini katika maji.
7.4 Yote hapo juu yaweza kufanyika katika
kuondoa chlorine kwenye maji lakini njia sahihi ni matumizi ya dawa maalumu aina
ya ……………… inayopatikana
madukani, japo ndani ya nchi yetu ni ngumu kuipata hivyo yaweza kuagiwa kutoka
nje ya nchi.
8.0 GHARAMA ZA UCHIMBAJI WA BWAWA:
8.3 Gharama za uchimbaji zaweza kuainishwa
katika makundi matatu; ushauri kutoka kwa wataalamu, gharama za uchimbaji na
gharama za kuandaa bwawa kabla ya kuweka maji na wakati wa kuweka maji.
8.4 Gharama
za uchimbaji wa bwawa zinatofautiana eneo kwa eneo na namna bwawa
linavyochimbwa, hii ikihusisha nguvu na vifaa vitakavyotumika.
8.2 Ni
vyema kuajiri watu kuchimba bwawa kuliko kutumia vifaa kama excavator, kama
bwawa ni kubwa sana waweza kutumia vyote kwa pamoja. Bwawa linahitaji
malekebisho mengi sana madogo madogo, hivyo matumizi ya watu kama nguvu kazi
katika kuyafanya hayo ni muhimu.
4.0 KUSAFISHA ENEO, UCHIMBAJI WA BWAWA
4.1 Mara
eneo linapochaguliwa, ni muhimu kuondoa majani, vichaka na miti yote. Mizizi
ing’olewe kabisa kwa kuwa itaoza na kuacha mashimo ambayo yatasababisha maji
kuvuja.
5.5 Mara eneo likisafishwa, bwawa lichimbwe kwa
vipimo sahihi ili kujua ukubwa wa bwawa. Hii itasaidia katika uchimbaji, kujua
ukubwa wa bwawa na idadi ya vifaranga watakao pandikizwa. Ni vyema kutumia
kamba ili kunyoosha ukuta wa bwawa wakati wa uchimbaji.
4.3 Matuta
yajengwe kwenye eneo lililosafishwa vizuri na ambalo halina mimea wala mawe kwa
ajili ya kuzuia kupotea kwa maji. Pia udongo wa juu ambao una majani na mizizi
usitumike kwa kutengenezea matuta ya bwawa.
4.4 Matuta
yasijegwe katika eneo la kichuguu kuzuia kupotea kwa maji, japo ni vigumu na
mara nyingine haiwezekani kabisa kuzuia uvujaji wa maji kwa aina hii.
8.2 Ni
muhimu kuhakikisha kwamba matuta yanajishikilia vizuri kwenye ardhi. Hii
inaweza kufanyika kwa kuchimba mfereji kuzunguka bwawa katikati ya eneo ambalo
matuta yatajengwa.
4.2 Matuta
lazima yashindiliwe vizuri kuzuia maji yasivuje. Njia rahisi ni kushindilia
matuta kila baada ya kuweka sentimeta 30 za udongo. Hakikisha udongo
unaloweshwa na kushindiliwa kwa kutumia kifaa chenye ubapa chini au kipande cha
mti. Ushindiliaji wa aina hii ni sawa sawa na ushindiliaji wa sakafu ya nyumba.
Ushindiliaji unafanya matuta kuwa imara na kutuamisha maji
4.0 Upana
wa tuta la bwawa inategemeana na ukubwa wa bwawa,ni vyema uwe na mita 3 chini na
mita 2 juu, mteremko(slope) katika ukuta wa bwawa ni kitu cha muhimu, hii ni
kupunguza mmomonyoko,na inamrahisishia mhusika kuingia ndani ya bwawa kwa
urahisi.
6.0 Kina
cha bwawa ni vyema kitofautiane, hii ikiwa ni futi 3-4 sehemu ya kina kirefu na
futi 1-1.5 sehemu ya kina kifupi. Eneo la kati lichimbwe katika namna
itakayowezesha kupata slope ya bwawa katika utofauti wa kina cha juu na chini.
10.1 Bwawa
likiwa na kina kifupi, itakuwa rahisi kwa maadui a samaki kukamata samaki. Pia
bwawa likiwa na kina kifupi litapata joto haraka wakati wa mchana na kupoa
haraka wakati wa usiku. Kwa hali hiyo joto la maji litabadilika sana kitu
ambacho ni hatari kwa samaki katika bwawa
10.2 Sababu
nyingine ya kuwa na kina kinachostahili
ni kwamba kwenye mabwawa yenye kina kifupi majani huota kwa kasi. Mimea kwenye
bwawa la samaki ina athari sawa sawa na mimea shambani.
10.3 Wataalamu
hawashauri kuchimba bwawa la kina kirefu kwa kuwa ni gharama, ngumu kulihudumia
na kuvuna samaki…………
5.5 Urefu wa matuta utategemea wingi wa udongo,
ukubwa wa bwawa na mfumo wa uvunaji wa samaki.
8.3 Ni
muhimu pia bwawa lijengwe katika namna itakayoruhsu kujazwa na kukaushwa kwa
maji kila inapohitajika. Hii ina maana kuwa maji yaingie bwawani sehemu
iliyoinuka na yaweze kutolewa wakati wa kukausha kupitia sehemu ya chini ya
bwawa.
5.4 Ili maji
yafike sehemu ya bwawa iliyoinuka, mfereji wa kuchepushia maji kutoka kwenye
kijito
utengenezwe.
5,3
Sehemu ya kuingiza maji iwekwe kwenye
kina kifupi na ile ya kutolea maji iwekwe kwenye kina kirefu kwa kuzingatia
picha hapo chini.
Outlet/inlet
Naitwa Mr. Abdul Lipoiye, ni mhitimu level ya Diploma katika mambo ya Ufugaji wa samaki toka chuo cha uvuvi mbegani mwaka 2013. Kwa anaetaka msaada kuhusu ufugaji wa samaki wasiliana nami kwa 0658530884 au email: manlipoiye@gmail.com.
ReplyDeleteSAWA KIJANA
DeleteAM Mudara Nehemia Christopherm,
Deletecompleted Diploma of environmental and coastal resource management from FETA 2014.
Honestly am so interested for good presentation of general overview on how to establish aquaculture project and all necessary procedures to reach and attain the targeted goals, as well as aquaculture aspects is concerned. I as stakeholder of this gigantic industry i take this opportunity to appreciate those who construct this document. I recommend that, let this be an a platform and opportunity door for those who are eligible expertise of aquaculture from different institutions so that to build capacity of implementation and provide consultancy service for those who are engaged in aquaculture firm to serve our communities.
nahitaji vifaranga
ReplyDeleteNaitwa Baraka Damas, nahitaji elimu ya kutosha kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara kwa mtaji mdogo na upatikanaji wa masoko. nipo morogoro mzumbe university 0654991662
ReplyDeletenatamani nianze mwezi december,2017 mtaji ninao lakini sijajua masoko na namna nzuri ya kufuga na chakula chake
ReplyDeletehi... Habari?
DeleteNAHITAJI VIFARANGA WA SAMAKI SATO MONOSEX.
ReplyDeletesawa unapatikana wapi
Delete